Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha. ( picha ya Maktaba )
Jana Feb. 26 2018 Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Dcp Charles Mkumbo Alipata ajali maeneo ya Mdori Minjingu Wilayani Babati Akitokea Mkoani Singida kikazi.
Rpc Mkumbo akiwa na dereva pamoja na msaidizi wake walikimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha Mount meru kwa ajili ya matibabu
Msumbanews Blog iliweza kuutafuta uongozi wa Hospital hiyo na kuweza kuzungumza Daktari Mfawidhi.
Daktari mfawidhi wa hospitali ya Mount Meru mkoa wa Arusha Jackline Urio amesema kuwa hali ya kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu kutokana na ajali aliyoipata.
Dokta Urio amesema kuwa walimpokea Kamanda mkumbo majira ya saa kumi akiwa katika hali nzuri na alipofikishwa hospitalini hapo aliteremka kwenye gari na alitembea mwenyewe mpaka wodini na alikuwa na ufahamu.
“Ni Kweli tumempokea RPC Kwenye saa kumi akiwa amepata ajali ya gari alikuja hali yake siyo mbaya sana alikuwa anajifahamu ameumia mkono kwa hiyo ilibidi alingia chumba cha upasuaji amefanyiwa upasuaji na wamefanikiwa kutengeneza mkono na anendelea vizuri”Alisema Dokta Urio
Post A Comment: