Wagonjwa waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya misiion ya Tenweek wamelazimika kuzikimbia wodi kuokoa uhai wao, baada ya jengo la hospitali hiyo kuwaka moto na kuteketeza baadhi ya majengo.
Hospitali hiyo ambayo ipo katika kaunti Bomet nchini Kenya, ilishika moto baada ya jiko la hospitali hiyo kulipuka na kuteketeza maeneo ya karibu ikiwemo store ya chakula na mgahawa, ambayo yako karibu na kitengo cha waonjwa mahututi na wodi kuu.
Akithibitisha kutokea kwa ajli hiyo Mkuu wa Polisi kaunti ya Samson Rukunga amesema jeshi la polisi limejitahidi kudhibiti moto huo usiathri sehemu kubwa na kuwahi kuuzima, na hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu
Post A Comment: