Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amefunguka kinachomvutia kutoka kwa mke wake Irene Uwoya msimu huu wa wapendanao (valentine).
Hitmaker huyo wa ngoma ‘Ngarenaro’ ameiambia ITV kwa sasa anavutika zaidi na mapishi ya mkewe.
“Vyakula anavyonikipia mke wangu hatari sana, fundi jikoni, mganga wa jiko. Ni wanamke mwenye vision, ni mtu ambaye tunaelewana, tunasikilizana, ni marafiki,” amesema Dogo Janja.
Dogo Janja na Irene Uwoya walifunga ndoa November mwaka jana, 2017 hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili ya ndoa hiyo kutokana na namna walivyoliweka suala hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: