Rukia Said akionyesha baadhi ya nyaraka zake zinazomtambulisha kumiliki eneo hilo kihalali.
Akionyesha hisia zake.
Mmoja wa watoto wa Rukia, Yahya Mbaruku akionyesha baadhi ya nyaraka zao zinazoonyesha umiliki wa eneo hilo.
Baadhi ya nyaraka ya malipo ya eneo hilo.


RUKIA Said ni mama mjane. Mapema leo alikusanya waandishi wa habari na kutoa kilio chenye kuumiza na kugusa kila mtu, machozi yake ni kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda, je ni nini kilichojificha nyuma ya machozi yake? Teremsha macho hapa chini.

Dhuruma. Ndiyo, mjane huyo anadai kudhurumiwa ardhi yake na mtu aliyemtaja kwa jina la Mohamed, eneo la Kigamboni na kwamba hana msaada zaidi ya kupiga magoti kwa serikali imsaidie.

“Imani yangu ni kwamba serikali hii ni ya wanyonge, nimedhurumiwa ardhi yangu na Mohamed tena mabavu na uonevu wa hali ya juu, nina vitu vyote muhimu vinavyothibitisha kwamba ile ni mali yangu, ikiwemo hati na risti ya malipo ambayo nimeyafanya kulipia ardhi, lakini leo anatokea mtu kwa sababu ana pesa na kinachoshangaza zaidi na yeye anadai kuwa na hati za ardhi yangu, huu ni utapeli mkubwa,” alisema Rukia na kuongeza;

“Ninaomba serikali inisaidie juu ya suala hili, Mkuu wa mkoa wetu ni mtu msikikivu wa vilio vya wanyonge kama mimi hivyo ninaomba alitazame suala langu ili nipate haki yangu, ninaomba sana kwani sina uwezo wa kupambana na huyu bwana.”

Naye kwa upannde wake, mmoja wa watoto wa Rukia, Yahya Mbaruku alidai kushangazwa na kitendo cha mama yake kudhurumiwa ardhi jambo ambalo limesababisha waishi maisha magumu.

“Eneo hili ni lile ukivuka tu feri upande wa Kigamboni, kuna maduka na vituo vingine vya biashara, ambavyo kwa kweli vingetuisaidia kusukuma maisha lakini jamaa huyo ametumia ujanja na mabavu yake kutudhurumu haki yetu, kama alivyosema mama kwamba tunaiomba sana serikali itusaidie ili tuweze kupata haki yetu,” alisema Mbaruku
Share To:

msumbanews

Post A Comment: