Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya Mbunge wa Mbeya mjini kuhukumiwa miezi mitano jela amesema kuwa ipo haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kuwaweka jela wote na kutorudia walichofanya kwa mbunge huyo.
Zitto Kabwe amesema leo kuwa ameona mashtaka ya Mbunge huyo yaliyopelekea kuhukumiwa jela miezi mitano.
Wabunge wa Upinzani tusimame kuhesabiwa sasa,
Nimeona mashtaka ya Sugu yaliyopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 5. Wabunge wote wa vyama vya Upinzani kwa namna moja ama nyengine tunasema haya kila wakati kwenye mikutano yetu. Kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kutusweka jela wote au kutorudia walichofanya kwa Sugu. Ninawasiliana na wenzangu tupate UNITED DEMOCRATIC FRONT,’ 
ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Facebook
Share To:

msumbanews

Post A Comment: