Meneja
wa label ya WCB, Sallam SK amefunguka kwa kuendelea kudai kw Fmamba
kampuni yao haina tatizo na chombo chochote cha habari isipokuwa Ruge
Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds FM na
Clouds TV ndio mwenye tatizo na label hiyo.
Mapema
wiki hii meneja huyo alianza kwa kuandika ujumbe mtandaoni unaodai kuna
mtu anataka kumshusha Diamond huku akidai hakuna mtu wa kumshusha
katika utawala huu wa Rais John Pombe Magufuli.
Sallam ameendeleza mashambulizi hayo ambapo jana amemtaja mtu aliyedai kwamba ana njama za kumshusha Diamond.
“Kwa
heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua
kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika
maovu yako yote unayoyafanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina
tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds Media Group ila
huyu Ruge Mutahaba ndio mwenye tatizo #TumekataaKuwaKaa,” aliandika
Sallam kupitia Instagram.
Meneja
huyo anaonekana kutaka kuendeleza harakati hizo kwani toka aanze kutoa
waraka huo amekuwa akiweka hushtag ambayo imekuwa ikitumika na Clouds
Media, #TumekataaKuwaKaa.
Ruge bado hajazungumza chochote kuhusiana na tukio hili
Post A Comment: