Klabu ya Mabingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imemuondoa mchezaji wake Yahya Zayd kwenye kikosi kinachotarajiwa kucheza leo dhidi ya Kagera Sugar FC baada ya kuugua ghafla mchana huu.
Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na klabu hiyo na kusema nafasi yake itachukuliwa na mshambuliaji Mbaraka Yusuph ambaye alipaswa kuanzia kutokea benchi.
Mechi hiyo ya Azam FC ni muendelezo wa michuano ya VPL mzunguko wa 18 ambao utapigwa katika dimba la Kaitaba mkoani Kagera.
Post A Comment: