Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameweka picha ambayo ina muonyesha Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu ambaye yupo Ubelgiji kupatiwa matibabu baada ya kushambuliwa risasi na watu wasiojulikana na Msaidizi wake Mh.Mbowe, Ben Saanane ambaye hajulikani alipo hicho ndio kitu kinachomuumiza.
Lema ameweka wazi kutoonekana kwa Ben Saanane ni kitu kinachouma sana pamoja na Mh. Lissu kuwepo hospitali.
“Kutoka kushoto ni Ben Saanane,Mimi Godbless Lema,Tundu Lissu na Wakili Peter Kibatala..Ben hajulikani alipo na Tundu Lissu yuko Hospitali.Inauma sana,” ameandika Lema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Post A Comment: