Mbunge Godbless Lema amefunguka na kutoa malalamiko yake bungeni kuhusu kitendo cha Bunge kugharamia matibabu ya Spika wa Bunge Job Ndugai nchini India huku Mbunge Tundu Lissu mpaka sasa kutogharamiwa matibabu na bunge.
Lema amewasha moto huo wakati wakijadili taarifa ya Utawala bora, Katiba na Sheria na kusema kitendo ambacho Bunge linakifanya si haki na si sawa kwani ni undumilakuwili kuwapa watu wengine haki huku wengine wakinyimwa haki hiyo ya msingi.
"Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa Spika Job Ndugai nafahamu yupo India kwa ajili ya 'checkup' na matibabu na vilevile Mhe. Lissu ambaye na yeye yupo Ubelgiji kwa ajili ya matibabu. Mhe Spika anatumia fedha za bunge na Serikali kwa ajili ya matibabu na ni mbunge wa bunge la Jamhuri ya Tanzania na Mhe. Lissu tumeendelea kumkusanyia pesa mitaani kwa vikopo na yeye vilevile ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii 'double standard' inayoendelea katika taifa hili kwamba Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anaweza kutibiwa na Serikali na Bunge na Mbunge anayetokana na upinzani aliyepigwa risasi Dodoma hawezi kutibiwa na bunge wa Serikali Mhe. Mwenyekiti Bob Marley ana wimbo unasema 'only time will tel'"
Lema aliendelea kusisitiza
"Chief yupo oposition kapigwa risasi, kifungu namba 24 section one ya Sheria ya uendeshaji bunge kinaeleza ni nani anapaswa kuwa na jukumu la pale inapotokea mbunge amepata matatizo na kama sitaweza kujadili maslahi ya wabunge siyo Lissu peke yake ya wabunge wote akiwa ameumia au hajaumia Mhe. nipo tayari nisiwe mbunge, kama sisi ni wabunge hatuwezi kujadili maslahi ya wabunge? Huyu anasimama anaongea mzaa hapa tunaogea kuna mtu amepotea anaitwa Ben Sanane na kuna watu wanapotea na haya mambo yanahusu utawala bora, Katiba na Sheria na haya mambo ni ya msingi kuliko madaraja, lami haya mambo tukiyajaili kwa mioyo tunajenga msingi imara kwa sababu kuna watu wamepotea kuna mtu ameumia yupo hospitali na tunapojadili hatuwashtumu tunataka mrudi kwenye mstari, mjue tunajadili damu za watu"
Post A Comment: