Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji ameibua tuhuma bungeni, akidai baadhi ya wabunge wamewatelekeza watoto wao na ni jambo ambalo amelishuhudia.
Akizungumza leo bungeni, Khatibu wakati wa kipindi cha maswali na majibu amesema kuwa chanzo cha watoto wa mitaani kimethibitika kwa sababu wanaume wengi wanashindwa kutunza familia zao.
Muheshimiwa mwenyekiti katika Bunge lililopita nilishuhudia binafsi hapa bungeni wanawake walileta watoto waliotelekezwa na waheshimiwa Wabunge, Je Mh. Mwenyekiti kupitia wizara ya afya uko tayari kwa wanawake wote waliotelekezewa watoto na waheshimiwa Wabunge wawalete hapa wakabidhiwe majukumu yao?,” amesema na kuhoji Khatibu.
Hata hivyo Mbunge huyo ameungwa mkono na mbunge wa Kavuu (CCM), Dk Pudensiana Kikwembe, aliyetaka jambo hilo kuwekwa wazi ili kujua kama wabunge hao wamezaa na wabunge wenzao au wamezaa na watu wengine lengo likiwa ni kujua jinsi ya kuwasaidia.
Katika ufafanuzi wake, Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile amesema kitendo cha kutelekeza watoto ni kinyume na sheria za nchi, kuwataka wananchi, hasa wanaume kuacha tabia hizo.
Hata hivyo, Naibu Waziri, Ndungulile amesema Bunge halina taarifa za wabunge kutelekeza watoto..
Share To:

msumbanews

Post A Comment: