Mbosso
Msanii wa muziki nchini Tanzania, Mbosso amewatangazia fursa ya kuonana na mashabiki wake nchini Tanzania leo Jumapili Februari 11, 2018. ambapo atawatembelea hadi majumbani mwao na kuwagawia CD ya nyimbo zake na kuwaimbia.
Mbosso ambaye yupo chini ya lebo ya WCB, amesema pia atatoa zawadi nyingine za vitenge na boksi moja la Diamond Karanga kwa kila familia atakayopitia kuwaimbia.
Siku ya kesho (jumapili) nimeitenga maalum kwajili ya kuja kuspend time na wewe Mdau Wangu, Maana wewe ni zaidi ya Ndugu yangu….Kuja kukupigia Gita huku nikikuimbia na familia yako pamoja na kukuachia CD yenye Nyimbo zangu Hizi Mpya Ambayo nitaisaini na Kuwapa kitenge kutoka kwa @Esmaplatnumz_ na Box ya @Diamondkaranga,“ameandika Mbosso kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Vigezo vya kupata nafasi ya kuonana na Mbosso ni kutembelea kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kisha acha comment kwa kuandika mtaa unaoishi, namba ya nyumba na kuacha namba yako ya simu kwa ajili ya mawasiliano.
Mpaka sasa Mbosso ameachia ngoma mbili tangu ajiunge na WCB na tayari wimbo wake mmoja umeshatazamwa na watu zaidi ya milioni moja.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: