Aliyekuwa mume wa Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akiwa safarini Arusha amekombwa kila kitu na majambazi nyumbani kwake Tabata Kimanga mchana kweupe.

Mtu wa karibu na Mbasha aliiambia Mikito Nusunusu kuwa, Mbasha alichanganyikiwa baada ya kurudi na kukuta amekombwa kila kitu cha ndani na majambazi.

Baada ya habari hizi kutua kwenye dawati la Mikito Nusunusu, lilimtafuta Mbasha ambaye alikiri kuibiwa kila kitu na kusema kuwa mpaka sasa amesharipoti polisi na uchunguzi bado unaendelea.

“Yaani sina la kusema walioniliza wamefanya kazi kwani wamechukua kila kitu cha ndani na kwa kweli wamenirudisha nyuma sana hata sielewi naanzia wapi,” alisema Mbasha.

Wakielezea tukio hilo majirani wa eneo hilo walisema kuwa mitaa hiyo mida ya mchana huwa ni tulivu sana kwani watu wengi huwa wanakwenda makazini ndio maana hata majambazi hao wakafanikiwa kuiba kila kitu bila kushtukiwa.

“Si unajua nyumba zetu ni za mageti makubwa mtu kujua moja kwa moja kuwa kwa f’lan kaingia mtu huwa si rahisi lakini tukio hilo limetokea kweli,” alisema jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Ali
Share To:

msumbanews

Post A Comment: