Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu ya Simba, Haji Manara ametoa wito kwa mashabiki, wapenzi na wanachama wa timu hiyo kuacha kuwazomea hasimu wao Yanga SC katika mchezo wao wa klabu bingwa Afrika raundi ya kwanza watakao cheza dhidi ya St Lous ya Seychelles.

Haji Manara ameyasema hayo kupitia kikao chake na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
“Natoa wito kwa washabiki wa Simba watakaoenda uwanjani kwenye mechi ya Yanga siku ya Jumamosi wasiizomee, tuzomeane kwenye ligi ya nyumbani..cc sote ni watanzania na tunawakilisha nchi,”amesema Manara.
Haji Manara ameyasema hayo wakati ambao timu ya Simba SC nayo ikikabiliwa na kibarua kizito siku ya Jumapili ambapo itaivaa Gendarmerie Nationale FC ya Djibouti.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: