TIMU ya Manchester united imeinyuka Huddersfield kwa bao 2-0, game iliyopigwa pale Old Traford jioni ya leo huku Romeo Lukaku na Alexis Sanches wakiing’arisha timu yao. 
Lukaku ndiye alikuwa wa kwanza kutupia bao la kuongoza la Man U kunako dakika ya 55 ya mchezo huo baada ya kumalizi krosi ya Juan Matta.
 
Game iliendelea huku mchezaji mpya wa Man U, Alexis Sanchez aliyenunuliwa klabuni hapo hivi karibuni akionyesha kiu kubwa ya kusaka bao na kuweka heshima klabuni hapo. 
Dakika 13, baadaye, Sanchez akatupia bao la pili ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.

Mpaka game inamalizika, Man U walikuwa wakiongoza kumiliki mpira kwa wasilimia 78 huku Huddersfield wakiwa na asilimia 28pekee.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: