Mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' amefunguka mazito kuhusu kushikiliwa kwa mtoto wake kwa kile kinachodaiwa kutoa lugha ya fedhea kwa Rais  na kusema yeye haoni kama amefanya kitu cha ajabu kwani hivyo ndivyo alivyo Sugu.
Mama mzazi wa Sugu alisema hayo Februari 4, 2018 alipotembelewa nyumbani kwake na Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema na  Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Katani ambapo kwa pamoja walikwenda kumtembelea Mbunge Sugu gerezani. 
"Miaka mingi sana toka yupo hapa anaimba miziki yake na kusemea matatizo ya nchi hii kwa hiyo hatushangai sana, mimi sioni kama amefanya kitu cha ajabu kwani hivyo ndivyo alivyo toka utoto wake ndiyo maana tulimwita Joseph mfanyakazi maanake ni mfanyakazi bora. Lakini anatetea haki kwa binadamu wenzie kuanzia yeye mwenyewe, watoto zake hata wajukuu zake watapata haki, anachotenda ni halali sana na hakuna tofauti" alisisitiza Mama yake na Sugu 
Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga Januari 25, 2018 walirudishwa rumande tena na kesi yao itaendelea Februari 8, 2018. Viongozi hao wanashtakiwa kwa kesi ya uchochezi. 
Share To:

Post A Comment: