Makamu wa rais wa zamani nchini Zimbabwe Joice Mujuru ameshambuliwa kwa mawe wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa siasa.
Chama cha upinzani cha Mama Mujuru cha National People's Party kimesema Bi Mujuru na wanachama wengine walishambuliwa kwa mawe walipokuwa wakifanya mkutano wa kampeni katika viunga vya mji wa Harare.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji BBC limesema kwamba msemaji wa chama hicho ameweka wazi kwamba mama Mujuru amejeruhiwa kidogo huku taarifa kutoka ndani ya chama ikisema watu wanane walijeruhiwa katika shambulio hilo.
Taarifa ya chama hicho imesema shambulio hilo lilikuwa la kisiasa na lilifanywa na wanachama wa chama tawala cha Zanu-PF Party.
Kwa upande mwingine Rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa, ameahidi kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo baadae mwaka huu na kuuhakikishia umma wa nchi hiyo kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.
Post A Comment: