Hali ya sito fahamu imeibuka mapema leo katika kikao cha pili cha robo mwaka wa fedha 2017 / 1018 katika Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Arusha Dc mkoani arusha

Hali hiyo imejiri mara baada ya madiwani wa chadema kugoma kuhudhuria katika kikao cha baraza hilo kwa madai ya kutotaka kushuhidia kuapishwa kwa diwani mwenzao wa Ccm kutoka katika kata ya Mussa Bi Flora Zelote aliyeshida katika uchaguzi mdogo uliyo pita pamoja na madai ya kutokulipwa posho zao za vikao viwili.


Hali hiyo imemladhimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Wilson Mahela  kulaani vikali hali hiyo na kufanya kuelekeza pesa za malipo ya leo zaidi ya shilingi milioni nane kupelekwa katika shule ya msingi yenye mahitaji muhimu ya kifedha katika  kata mbali mbali kwaajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi pamoja na ujenzi wa madarasa  katika halmashauri hiyo.


Mkurugenzi mahela ameeleza kuwa madiwani wa chadema kwa kuongonzwa na mwenyekiti wao Noah Lembris wasinge takiwa kugoma kujadili maswala ya maendeleo ya wananchi na badala yake kuweka fedha mbele kitu ambacho hakina maslahi kwa wananchi waliyo wachagua kuwawakilisha.


Nae kwa upande wa madiwani wa Ccm wakiongonzwa na Diwani wa viti maalum Mh Yasmini Bachu, Ameeleza kuwakupitia madai au sababu za malipo zinawahusu madiwani wote na kusikitishwa na madiwani wa chadema kugoma kitu ambacho amesema ni ukwamishaji wa maendeleo ya wananchi ili kutekeleza ilani ya awamu ya tano.


Aidha pia Mh Bachu ameongeza kuwa kikao hicho kilikuwa na ajenda muhimu za kujadili na kupitisha baheti mbali mbali mbali za kiutendaji wa serikali na kusema kuwa tabia hiyo haivumiliki na wapo tayari hata baraza hilo kuvunjwa kwani timu ya mkurugenzi na watalamu wake wanaweza kufanya kazi wanazo zifanya madiwani hao na mpaka pale uchaguzi mkuu utakapo fanyika ili wananchi waweze kuchuuja upya viongozi wawakilishi wanao wahitaji kwani hawa wa sasa wameshindwa kwenda na kasi ya Rais Magufuli.


Mara baada ya kumwapisha diwani mteule wa kata ya Musa Bi Flora Zelote mwanasheria wa serikali wa Halmashauri hiyo Dostan Shimbo alisoma kifungu cha sheria kwa kuahirisha kikao hicho cha baraza kutokana na idadi kutokutimia ili kujadili ajenda mbali mbali za maendeleo kwa wanachi na mwishowe Mkurugenzi alihairisha kikao hicho kilichokuwa kifanyike leo na kutokuhudhuliwa na madiwani wa chadema.


Nae kwa upande wake mwekiti wa baraza hilo la madini Noah Lembris amesema kuwa sababu kubwa ya kuto kuhudhulia kikao hicho ni kutokana na dharula kwa madiwani wengi kutoa hudhulu ya misiba na kueleza sababu nyingine ni kutokana na dharula za kawaida kutokana na maeneo yao wanayo toka na kukanusha kwa taarifa za kususia kikao hicho kwa sababu ya kudai posho zao.


Ikumbukwe bara la masiwani wa halmashauri ya Arusha inaundwa jumla ya madiwani 35 pamoja na M'bunge na kuwa na idadi ya watu 36 ikiwa madiwani 20 niwa chadema kupitia kata huku madiwani 7 niwa Ccm kupitia kata na wale wa viti maalumu chadema madiwani 7 na huku Ccm madiwani 2 wa viti maaalum.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: