Image result for MHESHIMIWA SUGU MAHAKAMANI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Februari 10, 2018 ameamuru washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga kuachiwa kwa dhamana ya milioni tano kwa kila mmoja. 
Kufuatia maaamuzi ya mahakama hiyo kesi inayowakabili Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi "Sugu" na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga itasikilizwa tena Februari 26, 2018 
Sugu na Masonga wanashtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Pombe Magufuli wanayodaiwa kuitoa Desemba 30,2017 na sasa washatakiwa hao wanatetewa na Wakili Msomi Peter Kibatala. 
Share To:

Post A Comment: