Klabu ya Coastal Union imerejea Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mawenzi.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Wagosi wa Kaya wamepata magoli kupitia kwa mkongwe Athumani Iddi ‘Chuji’ na Raizin Ally.
Kwa ushindi huo Coastal Union imefikisha alama 26 na kusalia nafasi ya pili kujihakikishia kurejea Ligi Kuu Vodacomn Tanzania Bara.
Timu nyingine iliyopanda daraja ni klabu ya KMC ya Jijini Dar es salaam baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mlale waliokuwa vinara wa Kundi B la Ligi Daraja la Kwanza.
KMC inaweka historia kwa kupanda Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa mara ya kwanza huku shujaa wake akiwa ni kiungo mkongwe Abdulhalim Humud aliyefunga bao hilo pekee lililoweka historia.
KUNDI B P W D L F A GD Pts
1. KMC 14 8 4 2 17 13 4 28
2. Coastal Union 14 7 5 2 18 9 9 26
3. JKT Mlale 14 7 4 3 13 7 6 25
4. Polisi Tanzania 14 6 6 2 18 12 6 24
5. Mbeya Kwanza 14 6 4 4 14 10 4 22
Post A Comment: