Yanga imeanza Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi kiduchu dhidi ya St Louis ya Shelisheli.
Sasa unatakiwa kwenda kumaliza kazi ugenini huko jijini Victoria na Kocha George Lwandamina anaamini watavuka.
Lakini Yanga ikifanikiwa kuvuka, lazima ifanye kazi ya ziada kujipanga maana itakutana na mshindi kati ya Township Rollers ya Botswana au El Merreikh ya Sudan.
Tayari nao wamecheza mechi ya kwanza na El Merreikh ambayo inaonekana ni kali, imevurumishwa mabao 3-0 ikiwa ugenini.
Kipigo hicho cha Merreikh kinaonyesha Rollers pia si timu ya kubahatisha na kinatoa salamu kwa Yanga kuwa itakutana na timu zilizo vizuri.
Kwani kama Merreikh watafanikiwa kupindua matokeo maana yake watakuwa imara kwa kiwango cha juu sana na kama Yanga watashinda na kukutana nao, basi haitakuwa mchezo.
Lakini kama watafanikiwa kusonga mbele, basi Rollers haitakuwa timu ya mchezo na hakika, Yanga wanapaswa kujipanga pia.

Post A Comment: