Kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite, 'Bilionea' Erasto Msuya (43) itaanza kunguruma tena leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi, baada ya kutengewa siku 23 za kusikiliza mashahidi wa upande wa Jamhuri.
Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi 22 Agosti 7, 2013, majira ya saa 6:30 mchana katika eneo la Mijohoroni, kando kando ya Barabara kuu ya Arusha-Moshi, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Jana, Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Bernard Mpepo aliithibitishia Nipashe kwa njia ya simu kwamba kesi hiyo namba 12 ya mwaka 2014, itasikilizwa kuanzia leo hadi Februari 28.
“Jaji Salma Maghimbi wa Arusha ambaye ndiye anayesikiliza kesi hiyo ameshafika Moshi na ratiba inaonyesha kwamba atafanya kazi hiyo kwa wiki tatu hivi, kuanzia kesho (leo) hadi mwisho wa mwezi huu," alisema Mpepo.
"Tunataka kesi hii ifike mwisho ndiyo maana tumeipanga kuisikiliza mfululizo.”
Kesi hiyo ya mauaji ya Bilionea Msuya ilianza kusikilizwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi Oktoba 4, 2015.
Mpaka sasa, mashahidi 33 kati ya 49 wanasubiri kutoa ushahidi katika kesi hiyo inayowakabili Sharif Athuman (31) ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mchimbaji mdogo, mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha na Shaibu Saidi maarufu kama “Mredii” (38), mkazi wa Songambele, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara.
Wengine ni Mussa Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu, Jalila Said (28), mkazi wa Babati, Karim Kihundwa (33), mkazi wa Lawate, Wilaya ya Siha na Sadiki Jabir a.k.a Msudani (32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata, wilaya ya Hai.
Pia katika kesi hiyo Alli Musa maarufu Majeshi, mkazi wa Babati, mkoani Manyara anashitakiwa kwa mauaji ya Bilionea Msuya.
Kwa wiki nne mfululizo, kati ya Oktoba 16 hadi Novemba 17 mwaka jana, Jaji Maghimbi alisikiliza mashahidi saba wa upande wa mashtaka na mashahidi wawili katika kesi ndani ya kesi.
Upande wa mashtaka katika kesi hiyo ambayo ni gumzo katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, unaongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdala Chavula.
Jopo la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo linaongozwa na Hudson Ndusyepo anayemtetea mshitakiwa wa kwanza, Majura Magafu anayemtetea mshitakiwa wa pili na wa tano, wakili Emmanuel Safari anayemtetea mshitakiwa wa tatu na John Lundu anayewatetea washitakiwa wa nne, sita na saba.

Post A Comment: