Kamati ya Maadili ya TFF iliyokutana Februari 3, 2018 na Februari 17,2018, katika ofisi za TFF Karume, Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa pia ilipitia na kutoa hukumu ya tuhuma za kutoa taarifa zisizo sahihi na kughushi leseni za usajili zilizowakabili watuhumiwa mbalimbali walioletwa mbele yake.
Tuhuma hizo zilitokana na mechi namba 26 kundi A Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika 29 Oktoba 2017 kati ya Mvuvumwa FC na Friends Rangers ambapo katika mchezo huo timu ya Mvuvumwa FC iliwachezesha wachezaji watano (5) ambao ni Elias Costa Elias (aliyevaa jezi namba 5), Lukwesa Joseph Kanakamfumu (jezi namba 7), Dunia Abdala Dunia (jezi namba 1), Doto Justine Kana (jezi namba 12) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi namba 8).
Post A Comment: