Fahamu kwamba ndizi mbivu ina faida kwenye urembo. Hili ni tunda ambalo lina wingi wa madini ya potassium. Madini haya yanasaidia kwa kiasi kikubwa kuifanya ngozi yako iwe na muonekano mzuri.
Je wajua kuwa maganda ya ndizi ni tiba ya chunusi? Kama unasumbuliwa na chunusi wala usipate shida kutafuta dawa zenye kemikali . Tumia tunda hili kupata ufumbuzi.
Ili kupata matokeo mazuri, chukua maganda ya ndizi na uyasugulie katika eneo ambalo limeathiriwa na chunusi. Hakikisha unasugua hadi ule weupe unapotea na rangi ya hudhurungi itaanza kutokea. Virutubisho vinavyotoka kwenye maganda hayo ndivyo vinavyokwenda kutibu chunusi na makovu.
Ukifanya zoezi hili angalau mara mbili kwa wiki utapata matokeo mazuri.
Maganda ya ndizi yanaweza kutumika kuondoa weusi kwenye kuzunguka macho. Saga ndizi mpaka ilainike kabisa kisha paka katika eneo unalotaka kuondoa weusi. Kama ngozi yako ni kavu changanya ndizi iliyosagwa na asali. Sugua mchanganyiko huo kisha uuache kwa dakika 15 mpaka 20 kisha nawa kwa maji baridi.
Ndizi inaweza kutumika kama kulainisha ngozi ya miguu pia. Unachotakiwa kufanya, isage ndizi ilainike na kisha uipake kwenye miguu. Kaa nayo kwa dakika 20 kisha nawa kwa maji safi ya baridi. Hii huifanya miguu kuwa laini na yenye kuvutia.
Post A Comment: