Katibu Tawala wa wilaya ya Arumeru Timotheo Mzava akishirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na Watendaji wa serikali wamefika katika kijiji cha Losinoni juu kilichopo Arumeru nakukuta mashamba makubwa ya bangi yakiwa yamechanganywa na Mahindi pamoja na Maharagwe.
Akiongea baada ya zoezi hilo Mzava ameagiza Watendaji wote wa Serikali ikiwemo Mtendaji wa Kijiji kukamatwa kwa kuhusika na kilimo hicho.
“Tumefyeka hekari 8 mpaka saivi hatujamaliza na hatujui tutamaliza saa ngapi, imelimwa kwa wingi imechanganywa kwenye mahindi na maharage, tumetoa maelezo kuanzia Mwenyekiti ambaye tutakuta Kijiji chake kinalimwa Bangi tutamchukulia hatua,” -Katibu Tawala Mzava
Post A Comment: