Klabu ya Tottenham imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya Arsenal mchezo wa ligi kuu ya Uingereza uliyopigwa katika dimba la Wembley.
Bao pekee la Spurs limefungwa na mshambuliaji wao hatari, Harry Kane kunako kipindi cha pili baada ya dakika 45 za awali kutoka sare ya bila kufungana.
Vikosi kamili vilivyo ingia uwanjani kwa upande wa Spurs ni Lloris (7), Trippier (7), Sanchez (8), Vertonghen (8), Davies (7), Dier (7), Dembele (7), Son (7), Eriksen (7), Alli (7), Kane (8).
Waliyokuwa benchi: Wanyama (5), Lamela (6).
Wakati kwa upande wa Arsenal: Cech (6), Bellerin (7), Mustafi (7), Koscielny (5), Monreal (6), Elneny (5), Xhaka (6), Wilshere (5), Ozil (6), Mkhitaryan (5), Aubameyang (5).
Benchi kulikuwa na  Iwobi (5), Welbeck (5), Lacazette (5).
Mchezaji bora wa mchezo huo ni: Harry Kane, kwa matokeo hayo yanaipeleka Tottenham hadi nafasi ya tatu kwa kuwa na jumla ya alama 52 ikizidiwa kwa pointi nne mbele ya Man United waliyopo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: