Fedha zilizotajwa kwa ni za misaada ya kijamii zimeibiwa wakati wa usafirishaji wa fedha hizo huko Ritavi karibu na Tzaneen nchini South Africa mapema leo. Taarifa hizo zimetolewa na Polisi wa Afrika Kusini.
Luteni Kanali Moatshe Ngoepe alisema kuwa tukio hilo limetokea kwenye majira ya saa 12 asubuhi ya leo.
“Watuhumiwa walipiga risasi gari hilo liliobeba fedha mara kadhaa na wakalipiga na bomu kabla ya kukimbia eneo hilo na kiasi cha fedha ambacho hakijulikani pamoja na silaha mbili ambazo waliziiba kutoka kwa viongozi wa usalama” alisema Luteni Kanali Moatshe Ngoepe.
“Hakuna majeraha au mauti yaliyotokana na tukio hili” aliongezea Luteni Kanali Moatshe Ngoepe.
Post A Comment: