Familia ya binti Akwelina Akwelini aliyepigwa risasi Februari 16, 2018 imefunguka na kuiomba serikali na viongozi wengine waweze kumsaidia mdogo wake wa Akwelina mwingine ambaye aliacha shule kidato cha tatu baada ya wazazi kukosa ada.

Msemaji wa familia hiyo Dismas Shirima ameishukuru serikali kwa kuweza kufanikisha mazishi ya binti huyo lakini pia amemshukuru Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa. Joyce Ndalichako kwa ahadi yake ya kumsomesha mmoja wa wadogo wa Akwelina na kusema kuwa familia hiyo hali yao ni duni hivyo kama watajitokeza watu wengine na kuguswa kumsomesha mtoto mwingine watakuwa wamesaidia kuwapunguzia machungu ya maisha wazazi wa Akwelina ambao walikuwa wakimtegemea sana binti huyo.

"Waziri aliahidi kumsomesha huyu binti mdogo na atakwenda kumsomesha sisi tumepokea kwa furaha kabisaa kwa maana atakuwa ameshaisaidia familia gharama za kumsomesha mtoto kiasi fulani familia itakuwa imepata aueni, sisi tulikuwa tunaomba kwa kuwa matatizo yapo mengi na si Waziri tu bali mtu yoyote yule anaweza kuona kuna umuhimu wa kuisaidia hii familia akaisaidia. Pamoja na watu na watu wanailaumu sana serikali lakini wao hakuna mtu ambaye ameonyesha uchungu wa kweli kwamba mimi nitafanya tukio ambalo litakuwa linaidaidia ile familia ili kuziba lile pengo ambalo ameliacha Akwelina kwa hiyo hawa viongozi wa serikali hasa Waziri ameshaonyesha hilo" alisema Dismas Shirima

Kwa upande wa binti huyo ambaye ni mdogo wa Akwelina alifunguka na yeye na kumuomba Waziri Ndalichako ili na yeye aweze kwenda shule kwani alikatisha masomo yake akiwa kidato cha tatu baada ya kukosa ada.

"Mimi nilishindwa kuendelea na masomo nikiwa kidato cha tatu mwaka 2016 kwa sababu ya kukosa ada, kwa hiyo naomba Waziri wa Elimu kwa jicho lake la huruma anisaidie na mimi anipeleke shule nitapambana kadri ya uwezo wangu na mimi nifikie alipofikia dada yangu Akwelina kielimu, nitashukuru sana kama atasikia ombi langu pia" alisema Hidaya Akwelina ambaye ni mdogo wa marehemu Akwelina
Share To:

msumbanews

Post A Comment: