Ikiwa ni siku moja imepita tangu Mahakama Hakimu Mkazi ya Mbeya kutoa hukumu ya kumfunga miezi mitano jela Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi hatimaye mzazi mwenzake, Faiza Ally amefunguka kwa kusema kuwa amechukizwa na kitendo hicho.
Picha inayohusiana
SUGU akiwa na Faiza Ally enzi hizo kabla ya kutengana.
Faiza Ally amesema kuwa kitendo hicho kimemuuma kama mzazi mwenzake ingawaje huwa maisha yake yanakuwa magumu zaidi pale Sugu anapokuwa uraiani.
Nikimuangalia kwenye maisha yangu namuona kama tu adui ambaye hana neno kwangu, kwahiyo mimi sina sababu ya kusema sijui namuhurumia sijui kapata matatizo shauri zake, hayo matatizo mimi kwa kweli naona akiwa uraiani maisha yangu yanakuwa magumu sana, sijali japo siombi akae jela hivyo, lakini saa nyingine unaona tu inabidi, aahh sijali kwa kweli,“amesema Faiza Ally kwenye mahojiano yake na Radio 5 kwenye kipindi cha Funiko Base.
Sugu amehukumiwa kwenda jela miezi mitano jana Februari 26, 2018 kwa kosa la kutoa maneno ya kichochezi na lugha ya fedheha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: