Mvinyo mwekundu awali ulihusishwa na faida mbalimbali za kiafya. kuanzia kupunguza hatari za kupata magonjwa ya moyo na kisukari, lakini sasa umebainika ni tiba ya meno.
Kwa sasa utafirti mpya unasema mvinyo huo una kemikali ambazo zinakabiliana na kuoza kwa meno na ugonjwa wa ufizi.
Watafiti walibaini kuwa mchanganyiko wa kemikali unaotengeneza kinywaji hicho, unaofahamika kama polyphenois, husaidia kumaliza na kuwamaliza vimelea (bakteria) hatari kinywani.
Lakini sasa watafiti hawa wanaonya kuwa matokeo ya utafiti wao hayatoi ruhusa ya ‘kunywa’ mvinyo kupita kiasi.
Utafiti wa awali ulionyesha kuwa faida za kiafya za polyphenois zilihusishwa na kuwa na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya vimelea hatari wanaoshambulia mwili.
Watafiti walilinganisha athari za aina mbili za kemikali ya polyphenois kutoka kwa mvinyo mwekundu dhidi ya mbegu za zabibu na kiasi kidogo cha mvinyo mbadala kwenye bakteria wanaoganda kwenye ufizi na meno na kusababisha magonjwa ya kinywa, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ufizi.
Walibaini kuwa kemikali ya mvinyo kwa pamoja vilipunguza uwezo wa vimelea kukaa kwenye seli, lakini kenikali za polyphenois – caffeic na p-coumaric acids – zilizofanya kazi bora zaidi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: