Leo ni 'Birthday' ya klabu ya Yanga ambayo inatimiza miaka 83 tangu kuanzishwa kwake, ikiwa ndio timu kongwe zaidi hapa nchini na ikiongoza pia kutwaa baadhi ya mataji ikiwemo ligi kuu.
Yanga SC ilianzishwa rasmi Februari 11, 1935 ambapo imepitia maboresho na mabadiliko kadhaa hadi sasa ambapo inatambulika na mashirikisho ya soka ya nyumbani na kimataifa kama (Young African) na kwa mashabiki wa hapa nyumbani ikifahamika kama Yanga.
Mbali na kuwa timu kongwe, lakini kwenye upande wa mafanikio Yanga ndio mabingwa wa historia wa Ligi kuu Tanzania Bara wakiwa wametwaa taji hilo mara 27, idadi ambayo haijafikiwa na klabu yoyote hata mahasimu wao Simba SC.
Mafanikio mengine ni kuwa bingwa mara 5 wa kombe la Kagame pamoja na kuwa bingwa mara 6 wa kombe la Muungano. Pia Yanga inajivunia kufuzu robo fainali klabu bingwa Africa mwaka 1998.
Hatua nyingine kubwa kwenye michuano ya kimataifa ni kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Africa mwaka 2016. Pia ndio timu ya kwanza kucheza klabu Bingwa Africa kutoka Tanzania mwaka 1969.
Post A Comment: