Aliyekuwa Katibu Kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbroad Slaa amefunguka baada ya katazo kwa vyama vya siasa kuendesha mikutano ya hadhara.
Dkt. Slaa ambaye kwa sasa ni Balozi amekiambia kituo cha runinga cha Clouds kuwa hakubaliana na jambo hilo kwa sababu uwepo wa mikutano hiyo ni kitu ambacho kilipitishwa na bunge.
“Mimi sikubaliani na jambo la kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa kwa jambo lililopitishwa na Mhe. Rais kwa maneno tu sababu Rais hafanyi kazi kwa maneno na hili jambo lilipitishwa na bunge iweje sasa mtu mmoja azuie,” amesema.
Katika hatua nyingine Dkt. Slaa amesema yeye ni muumini wa Demokrasia na anapenda uwepo wa vyama vingi ila muelekeo wa kisiasa nchini kwasasa haumfurahishi.
“Mimi nilijiuzulu siasa ya vyama vingi pia katika tafsiri yangu huwezi kuachana na siasa sababu ni maisha, lakini nilisema kuwa nitakuwa tayari kupigia kelele jambo lolote lile lenye maslahi kitaifa,” amesema Dkt. Slaa.
Post A Comment: