Waziri wa mambo ya ndani ya nchi amewataka wanasiasa kuacha kutumia kuumia kwa mbunge Tundu Lissu kama chambo ya kisiasa katika majukwaa.

Dr mwigulu amesema hayo jana mkoani Singida wakati wa kampeni za udiwani kata ya Mitunduluni.

Dr Mwigulu  amewataka waache kutumia matatizo ya ndugu yao kama mitaji ya kisiasa badake yake waje na hoja za maana za kusaidia katika maendeleo ya nchi.

Aliongeza kusema kuwa mwaka uliopita uhalifu wa ajabu ulitokea ambapo kuna watoto wadogo wa chekechea walitekwa na kuuwawa ambao hawakuwa na hata shida na mtu yoyote na wazazi wao ni watu wa kawaida kabisa je serikali ndio imehusika.

"Sisi tunaoshughulika na maswala ya uhalifu tunatafuta wahalifu wanaofanya mswala ya kihalifu, kuna watu wanaona ni ajenda ya kisiasa wakati sisi tuombea mtu apone" alisema Dr Mwigulu

Dr Mwigulu ameongeza kusema kuwa je angeamua kuendelea  kusema kuhusu kupigwa risasi kwa mwanajeshi masaki inauhusiano gani na shida za kata ya mitundulini, hivyo wananchi wa singida wawaadhibu kwa kuwanyima kura katika uchaguzi wa tarehe 17 mwezi huu.

Uchaguzi mdogo katika kata ya mitunduluni unafanyika baada ya Diwani aleyekuwepo katika kata hiyo kufariki dunia kwa maradhi.​
Share To:

msumbanews

Post A Comment: