Diwani wa Chadema wa Kata Bagara  Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Ndg. Nyeusi Boniface  
amejivua udiwani pamoja na nyadhifa zake zote kisha kutangaza kujiunga na CCM.

 Ndugu Nyeusi amesema kuwa kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa kiongozi kupitia upinzani wa Tanzania lazima kwanza ujifunze unafiki, upotoshaji na uongo, amesema huwezi kuthaminiwa ndani ya upinzani iwapo huna hizo sifa.

Amesema kuna wakati wanatishia vikao na kufundishwa namna ya kukabiliana na serikali ktk kukwamisha jitihada zozote za maendeleo maana serikali ilifanikiwa kutekeleza ahadi zake kwa ufasaha ina maana upinzani hautakuwa na cha kuombea kura.

Nyeusi amesema kila Mwerevu anajua kuwa miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa ktk kila kona ya nchi inatekelezwa na serikali kwa kutegemea na mipango ya maendeleo kadri ya upatikanaji wa fedha na siyo fedha binafsi za madiwani wala wabunge.

Lakini hakuna mbunge wa Chadema wala Diwani wa CHADEMA anayeruhusiwa kuwaambia wananchi kuwa miradi hiyo inatekelezwa na serikali ya CCM, wanatakiwa kupotosha na hata kukwamisha ili isije kuonekana kuwa serikali ya CCM ndiyo inayafanya hayo.

Nyeusi amesema ukiwa upinzani, kitendo cha kupongeza au hata kuunga mkono hadharani juhudi za Rais mzalendo wa Tanzania unaitwa msaliti, lakini kila Mtanzania mwenye macho anaziona jitihada za Mh Rais Magufuli, hata wanasiasa wakijaribu kupotosha bado historia itajiandika siku moja.

"kwasababu hauruhusiwi kupongeza chochote wala kusifia chochote kizuri ikiwa kimefanywa na serikali, na hata Lowasa alipojaribu kupongeza mazuri alianza kuitwa msaliti, mimi sitaki kuwa mtumwa wa uhalisia. Ninaikumbuka Tanzania ya juzi, nimeiona Tanzania ya jana, na ni ninaiishi Tanzania hii ya leo, siwezi kuwa mnafiki na kuendelea kupotosha na kupinga kila kitu kwa amri ya viongozi wa chama" amesema Nyeusi
Share To:

msumbanews

Post A Comment: