Pichani ni Diwani wa kata ya daraja mbili Mh Prosper Msofe akiwa amepanda gari la polisi ili kupelekwa katika kituo kikuu cha.polisi mkoa wa Arusha kwa mahojiano zaidi.

Diwani wa kata ya daraja mbili katika jiji la Arusha Prosper Msofe amekamatwa na jeshi la polisi baada ya kikao cha baraza la madiwani kilichokuwa kikifanyika katika ukumbi wa baraza hilo jioni hii akituhumiwa kumiliki nyaraka za siri za mikataba ya wafanya biashara wa stendi ndogo na halamashauri hiyo.



Tukio hilo ambalo limewashangaza madiwani wengi  waliokuwa kwenye baraza hilo tukio hilo limetokea majira ya saa 11 Jioni baada ya askari polisi takribani 8 wakiwemo waliovalia kiraia kuvamia ukumbi wa mikutano na kuanza kufanya upekuzi kwenye mikoba ya madiwani hao ikiwemo ya kike wakisaka nyaraka hizo kitu ambacho madiwani wengi hawajakipenda kusachiwa pasipo idhini yao.


Mara baada ya jeshi la polisi kukamilisha zoezi la upekuzi na kuonekana kuzikosa nyaraka hizo ndani ya ukumbi huo waliondoka na diwani huyo  na kumpakia kwenye  gari lenye namba PT 1222 aina ya landrover.


Hayo yamejili mara baada ya diwani Msofe  kumtuhumu Mkurugenzi wa jiji pamoja na Meya wa jiji  kusaini mkataba na wafanyabiashara wa maduka eneo la stand ndogo kinyume na maazimio ya baraza hilo na kudai anazo nyaraka za mikataba hiyo iliyosainiwa jambo lililosababisha Mkurugenzi kuhoji upatikanaji wa nyaraka hiyo kitu ambacho alisema hajawahi kusaini mikataba kinyume na makubaliano ya baraza hilo la madiwani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: