Huku akiwa ameambatana na mwanasheria wake, Diamond amewasili mahakamani hapo saa 5:30 asubuhi akiwa katika gari namba T709 DLU aina ya Land Cruiser Prado rangi ya bluu mpauko.
Baada ya kuwasili katika viunga vya mahakama hiyo, alipitiliza moja kwa moja hadi katika mahakama ya watoto iliyopo ndani ya mahakama hiyo.
Saa 5:42 Mobeto ameingia mahakamani hapo akiongoza na watu wawili.
Mobeto na Diamond wapo katika hatua ya kutafuta suluhu ya matunzo ya mtoto, Prince Abdul katika mahakama hiyo upande wa watoto.
Post A Comment: