Msanii wa muziki, Diamond Platnumz Jumatatu hii amekabidhiwa leseni ya kurusha matangazo ya vituo vyake vya Wasafi Redio na Wasafi TV na Mhe. Waziri wa Habari, Tamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma.
Hatua hiyo inaonyesha huwenda vituo hivyo vikaanza kurusha matangazo hivi karibuni kutokana na maandalizi mengi kufanywa.
Diamond amepost ujembe huu instagram.. Leo tulikabidhiwa Rasmi Leseni ya @wasafitv na @wasafifm na Mh Waziri wa Habari, Tamaduni , Utalii na Michezo Zanzibar mh Rashid Ali Juma…..Shukran Nyingi ziifikie Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Jamuhuri nzima ya Muungano wa Tanzania… Ma raisi zetu pendwa Dr John Pombe Magufuli & Dr Ali Mohammed Shein pamoja na Mawaziri wa Habari Tamaduni na Michezo Mh Rashid Ali Juma & Harrison Mwakiyembe….Tamanio letu ni kutengeneza nyanja za Ajira kwa nduguzetu wenye Taaluma za Habari na Utangazaji ambao pengine hawajapata nafasi bado….kwa kuthamini kuwa, bila wao leo hii sisi tusingekuwepo….lakini pia Pamoja kushirikiana na Media zetu nchi Kuendeleza kunyanyua Vipaji toka mitaani na Tasnia nzima ya Sanaa, Michezo na Tamaduni…. #HiiNiYetuSote
Share To:

msumbanews

Post A Comment: