Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kusitishwa kwa kampeni ili kujumuika katika mazishi ya Kingunge Ngombale Mwiru.
Hayo aliyasema kwenye kampeni za kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kinondoni Salum Mwalimu kwenye viwanja vya Kinondoni manyanya.
Mbowe alisema Kingunge ni mtu alifanya mengi kwenye taifa hili kutokana na uadilifu wake na kesho kwa pamoja tunamsindikiza.
"Mzee Kingunge ni mtu mwadilifu amefanya mengi kwenye taifa hili alikuwa CCM na baadaye Chadema kesho tutasitisha kampeni ili kushiriki maziko" amesema Mbowe.
Naye mgombea ubunge Mwalimu amesema vipaumbele vyake ni vitatu ila atakapochaguliwa ataanza na elimu pamoja na afya.
"Najua kata nyingi hazina vituo vya afya wala shule za kata mtakaponichagua kipaumbele changu cha kwanza nitahakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya na shule ya sekondari" alisema Mwalimu.
Post A Comment: