Kuelekea uchaguzi mdogo wa marudio unaotarajiwa kufanyika Februari 17 mwaka huu, chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kunasa mpango wa wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuwapanga vijana wa Uvccm kusimamia vituo vya kupigia kura nje ya utaratibu ambao unataka wasimamizi wa kura waombe nafasi hizo na wateuliwe kwa muujibu wa sheria za uchaguzi.
Akiongea na waandishi wa habari leo Februaru 11 2018, Mkurugenzi wa operesheni na mafunzo wa chama hicho Benson Kigaila, ameyasema hayo na kuongeza kuwa hawatawaacha salama wakiwakuta Uvccm wakisimamia uchaguzi.
“Tukiwakuta vijana wa Uvccm ama viongozi wa CCM wakisimamia uchaguzi wa kinondoni hatutawaacha salama na tunaomba walitambue hili kabisa”. Bensoni.
Vilevile wamelalamikia msimamizi wa uchaguzi kushindwa kuwaapisha na kuwapa fomu za uwakala mawakala wa chama chao
Amesema kuwa malalamiko yao wamewasilisha kwa mwanasheria wa tume ya uchaguzi na kuwaahidi kuchukua hatua lakini sasa hapokei simu.
Amesema kuwa wanamhitaji mkurugenzi na msimamiz wa uchaguzi kinondoni awaeleze sababu kwanini hajatangaza majina ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura kitendo ambacho ni kinyume na taratibu za uchaguzi zinazowataka wasimamizi wawe wanatambulika siku kumi na nne kabla ya uchaguzi.
Kufuatia habari waliyopewa na Mkurugenzi wa manisipaa ya kinondoni ya kuongezeka kwa vituo vya kupigia kura, Kurugenzi ya usimamizi wa uchaguzi ndani ya chama wanahoji vituo hivyo vitasimamiwa na mawakala gani na kwa utaratibu upi.
“Tunajiuliza hivi vituo vitasimamiwa na mawakala gani na wapiga kura wake watatoka wapi”. amesema Benson kwa kauli ya kuuliza.
Amesema kuwa CHADEMA, wanauchukulia uchaguzi wa kinondoni kama kipimo cha kuionyesha serikali juu ya namna walivyojipanga kulinda Demokrasia ndani ya nchi.
Aidha Saidi kubenea ameaema kuwa kwa tadhimini ya uchaguzi inaonyesha Chadema wako juu kwa 67%, hivyo wameshashinda wanachohakikisha ni kutangazwa na hawatakubali kuona haki yao inadhulumiwa.
Ameongeza kuwa wanatangaza kutomwamini mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kwa madai kuwa Mkurugenzi wa manispaa ya kinondoni anapewa na maelekezo na mwenyekiti huyo wa tume namna ya kuhujumu uchaguo huo.
“Mwenyekiti wa kampeni zetu za Chadema, Fredrick sumaye amekaa kwenye uwaziri mkuu miaka kumi hivyo ana watu serikalini wanaotupa kila kitu kuhusu hujuma zinazopangwa”. Amesema kubenea.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: