"Ajenda ya ufisadi ndio ilikuwa ajenda kuu ya CHADEMA iko wapi sasa hivi. Leo tunazungumzia suala la Katiba mpya je Katiba yenu ya chama mnaitekeleza kwa asilimia 100, kama Katiba yako mwenyewe inakushindwa utaweza kuheshimu nyingine. Kwa hiyo ni lazima tuheshimu Katiba zetu za vyama na tuoneshe kweli tunazifuata na utaratibu huo ili sasa tuende hata kudai Katiba mpya tujenge hiyo misingi", alisema Katambi.


Pamoja na hayo, Katambi aliendelea kwa kusema "kwa dhamira ya uzalendo mimi na sema hapana lazima wajitafakari upya na kujijenga na ingekuwa bora zaidi hata wangepoteza muda mwingi katika kipindi hiki kujijenga kuliko hata kwenda kufanya uchaguzi. Gharama wanazozitumia sasa kwenye uchaguzi wangezitumia kwenye kujijenga kama taasisi kuboresha chama kionekane".


"Vyama vya upinzani hasa CHADEMA mimi naweza kusema kimepoteza muelekeo, kimebadilishana koti kwa maana ajenda tulizokuwa tunasimamia hatusimamii tena sasa zinasimamiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)", alisema Katambi", alisisitiza Katambi.
Kwa upande mwingine, Katambi amesema hakuna jambo jema walilowahi kufanya vyama vya upinzani bali wanachofanya wao ni kukosoa na kuipinga serikali katika mambo mema wanayoyafanya
Share To:

msumbanews

Post A Comment: