Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Anne Kilango Malecela jana Februari 5, 2018 amefunguka na kuwahakikishia Watanzania kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitashinda katika uchaguzi wa marudio katika jimbo la Siha lililopo mkoani Kilimanjaro.
Anne Kilango amesema kuwa ana uhakika kuwa jimbo hilo safari hii lazima litarudi CCM na kudai kuwa yeye mwenyewe alhamisi anakwenda Siha kuongeza nguvu na kuhakikisha ushindi unapatikana.
Mbunge huyo kwa kujiamini kabisa akiwa Bungeni leo amewathibitishia Watanzania kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitashinda jimbo la Siha lakini hakuzungumzia kabisa kuhusu jimbo la Kinondoni ambalo pia Februari 17 litafanya uchaguzi wa marudio ilihali chama chake hicho pia kinashiriki katika uchaguzi huo, jambo ambalo linafanya watu waanze kujiuliza chama hicho kimekata tamaa kushinda katika uchaguzi huo wa Kinondoni?
"Alhamisi ya wiki hii mimi nahamia Siha na naomba Watanzania wawe na uhakika kwamba Siha litakuwa jimbo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Naibu Spika naomba nikuhakikishie kwamba CCM inashinda Siha" alisisitiza Anne Kilango Malecela
Mbali na hilo Mbunge huyo aliiombea Wilaya hiyo ya Siha kwa Waziri wa Nishati na Naibu Waziri ili iweze kupata umeme katika maeneo ambayo bado hayajapata umeme ili yaweze kupata umeme kipindi hiki.
Wananchi wa jimbo la Siha na Kinondoni wanategemea kufanya uchaguzi wa marudio Februari 17, 2018 kuchagua wabunge ambao watawawakilisha kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post A Comment: