Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya ametangaza vita katika Jimbo la Kinondoni huku akiapia kwa Mungu wake kuwa atalinda kura za mgombea wao na lazima atangazwe mshindi kwa madai wamejipanga vilivyo.
Bulaya ametoa kauli hiyo zikiwa zimebakia takribani siku nne pekee kuelekea marudio ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Siha na Kinondoni ili wananchi wa maeneo hayo kupiga kura kwa mtu anayemuhitaji kuwa muwakilishi wake katika jimbo.
Bulaya amesema kuwa “Haki ya Mungu, Baba wa Taifa angekuwa hai angetoka CCM kwa sababu CCM ile sio hii ya sasa ambayo haifuati utaratibu, poleni wanaccm wenzangu wa zamani mmedharauliwa kwa kutoshiriki kura za maoni kumpata Maulid Mtulia. Baba wa Taifa alikuwa haendekezi vitu kama hivyo, lakini anafanya hivyo akiamini kabisa wanakinondoni mtachagua mgombea mnaemtaka halafu watatumia nguvu”.
Pamoja na hayo, Bulaya ameendelea kwa kusema “haki ya Mungu ngojeeni niwaambie hii ni ‘game’ ni sawa na ‘Escape from Sobibor’ yaani tunapiga kura, tunalinda kura na lazima mtu atangazwe. Sisi kule kwetu tunasema vita ni vita mura na nipo hapa lazima mtu atangazwe, polisi wananisikia yaani mara mia wao wahamishe kituo chao lakini sisi mtu wetu lazima ashinde.  Tumerudi kwa kujipanga”.
Kwa upande mwingine, Bulaya amewataka wananchi wa jimbo hilo kutorudia kosa kwa kumchagua mtu ambae atawarudisha tena kwenye sakata la uchaguzi kama ilivyokuwa sasa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: