Benki kuu ya Tanzania imeyafungia maduka 86 ya kubadilishia fedha za kigeni baada ya kushindwa kutimiza masharti ikiwemo kutoa vielelezo vinavyoonyesha fedha za kigeni zinazotumika kwenye biashara hiyo zimetokana na chanzo kipi.
Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya kuandika habari za kiuchmi mkoani Mtwara meneja wa kitengo kinachosimamia fedha za kigeni kutoka benki kuu ya Tanzania Eliyamringi Mandari amesema kufungwa kwa maduka hayo kunatokana na oparesheni inayoendelea nchi nzima kwa sasa yenye lengo la kuleta ufanisi wa kazi katika maduka hayo.
Amesema upareresheni hiyo inakwenda sambamba na usajili upya wa maduka hayo ya kubadilisha fedha za kigeni ambayo imetokana na kanuni mpya ya kusimamia maduka hayo lengo hasa ni kuongeza ufanisi na mitaji katika kuendesha biashara hiyo.
Hata hivyo amesema katika oparasheni hiyo maduka 297 yametuma maombi yao huku maduka sitini na tano yanaendelea kufanyiwa kazi, sabini na moja tayari yamepatiwa leseni mpya pamoja na matawi yake arobaini.
Amesema maduka 86 yamefutiwa leseni kutokana na kushindwa kutimiza masharti ikiwemo kueleza vyanzo vya mitaji inayotumika katika kuendesha.
Biashara hiyo na kusisitiza wiki mbili zijazo zoezi hilo litakamilika na taarifa kamili itatolewa.
Kufuatia opareheni hiyo mandari amesema ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuendesha biashara ya fedha za kigeni bila leseni ya benki kuu adhabu yake ni faini shilingi milioni nne, ama kifungo cha miaka kumi na nne gerezani, ama vyote viwili.
Source: ITV
Post A Comment: