STAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kuwa Moses Iyobo ambaye ni mzazi mwenziye hashtushwi hata kidogo na picha anazopiga akiwa amevaa mashuka na za nusu utupu kwa sababu anajua ni kwa ajili ya kibiashara tu.
Akizungumza na Mtandao huu Aunt, alisema kuwa mara nyingi hata picha ambazo anapiga na Iyobo anakuwa pembeni kwa maana ni za matangazo ya sabuni yake hivyo hawezi kuvaa nguo ya kawaida anapokuwa bafuni zaidi ya taulo kuonyesha uhalisia.
“Iyobo hawezi hata siku moja akazishangaa picha hizo kwani ni za matangazo nazoziweka mtandaoni, maana anajua kabisa ni za kazi na si za kitu kingine chochote kile kwa maana hata yeye anakuwepo na anatoa mawazo mbalimbali katika picha hizo zipigwaje,” alisema Aunt Ezekiel.
Post A Comment: