Diwani wa Kata ya Sombetini, Ally Bananga amemuonya mgombea Ubunge wa CHADEMA jimbo la Kinondoni ndugu, Salum Mwalimu kufahamu kuwa kama atakuja kuwasaliti baada ya kushinda uchaguzi kwa kuhama chama ajue hataweza kuwa salama katika maisha yake.
Diwani Bananga ameyasema hayo akiwa katika Kata ya Ndugumbi Kagera Kinondoni jijini Dar es salaam ikiwa ni katika muendelezo wa kampeni za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17 na kusema kwamba anamkumbushia suala hilo mgombea kwavile wanafahamu kuwa msaliti hana alama.
"Tunarudia Kusema Maana Msaliti Hana alama. Kama utakuja kutusaliti Salum hutakuwa salama wewe, watoto wako na hata wale mbuzi wako hawatabaki salama. Hatuna muda wa kuchekecheka na wala hatutarudia uchaguzi kwa mambo ya kipuuzi" Bananga.
Bananga amemtahadharisha mgombea huyo kufahamu kwamba kuwa kwake mbunge wa jimbo la kinondoni ni kama vile kufunga ndoa na wana kinondoni hivyo anatakiwa kuwafikisha wananchi hao mahali ambapo walikuwa wanatarajiwa kufikishwa na Mbunge aliyejiuzulu (Mtulia).
Mbali nayo Bananga amemtaka mgombea Mwalimu ahakikishe anakuwa bega kwa bega na wanakinondoni kwenye matatizo na raha zao na pale anapohitajika.
Post A Comment: