Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuwanoa viongozi wake kwa kuwapa mafunzo ya Itikadi na uongozi huku mafunzo hayo yakiwahusu pia wanachama na wananchi wa kawaida ambao wanatakiwa kukifahamu vyema chama hicho.
Akizungumza na mtandao wetu leo, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndugu Ado Shaibu amesema “Siasa ya nchi yetu ina maradhi kadhaa, Kwanza siasa zetu hapa nchini si za masuala. Pili kwenye vyama vyote hakuna mkazo mkubwa katika kuielewa Itikadi ya chama husika kwahiyo mafunzo hayo yanaklenga kuwa tiba ya maradhi hayo,” amesema Ado.
Aidha Ado amesema kuwa mafunzo hayo yataanza rasmi siku ya Jumamosi Februari 10 mwaka huu na yatatolewa kwa muda wa miezi miwili.
Post A Comment: