CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema viongozi wake wa ngazi za juu watafanya ziara katika mikoa kadhaa nchini kuanzia Februari 12 hadi 25 mwaka hu ili kuimarisha muundo na uhai wa chama hicho.
Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Ado Shaibu, aliyasema hayo leo wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
Akifafanua, alisema Mwenyekiti wa chama hicho, Yeremia Maganga atafanya ziara hiyo katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani Tanga, Arusha na Kilimanjaro ambapo ataambatana na Katibu wa Kampeni na Uchaguzi, Mohammed Massaga.
Naye Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Shaaban Mambo ataambatana na Naibu Katibu Mkuu Bara, MsafiriMtemelwa, na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ado Shaibu, ambapo watafanya ziara mikoa ya Dodoma, Singida, Geita, Simiyu na Kagera. Ziara hiyo itafanyika kuanzia Februari 14 hadi Februari 23 mwaka huu.
Shaibu pia alitoa wito kwa wananchi wanaopenda kujiunga na chama hicho, kufanya hivyo kwenye vikao vya viongozi hao pindi watakapofika kwenye maeneo yao.
Post A Comment: