Yanga ni kama wameonyesha dhamira mapema ya kuwaua Azam siku ya Jumamosi licha ya Kuwa watu wengi wanabeza kikosi chao kwasasa kutokana na aina ya matokeo wanayoyapata kwasasa.
Yanga ambao wapo nafasi ya 3 katika msimamo kwasasa wakiwa nyuma ya Azam Fc na Simba wanaoongooza Ligi wamejipanga kwa mambo makubwa 3 wiki hii kuelekea mchezo kati yao na Azam Fc.

Kuingia Kambi na Kufanya Siri juu ya Kambi

Yanga  wameingia Kambini toka juzi siku ya Jumapili huku wakigoma katakata kusema kuwa kambi yao iko wapi licha ya leo kuonekana wakiendelea na mazoezi yao kama kawaida katika uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam ambao wamekuwa wapinzani wao wakubwa miaka ya hivi karibuni kutokana na Ubora wa Vikosi cha timu hizo.

Akiongea Nasi mwenyekiti wa kamati ya mashindano Hussein Nyika amesema Wanajua kuwa mechi itakuwa ngumu lakini wanajipanga kuhakikisha wanapata ushindi na Nyika akasisitiza Kuwa timu iko kambini na Kambi inabaki kuwa siri ya Klabu.

Wakongwe waungana kutaka kuwaweka sawa wachezaji.

Baadhi ya wachezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga wamejipanga kwenda Kuongea na Wachezaji wa Yanga ili kujua tatizo hasa ni nini wa timu kutocheza vizuri na kama kutakuwa na matatizo ambayo wachezaji wanashindwa kuongea na viongozi basi wachezaji hao wawaambie wachezaji hao wa zamani.
Lengo la Wakongwe kuongea na wachezaji pia ni kuwaongezea madini na kuwafanya kuongeza morali wawapo uwanjani na mambo kama hayo.


MALIPO YOTE KUMALIZWA MWISHO WA MWEZI

Kulingana na chanzo cha ndani Klabu ya Yanga inaelezwa kuwa wachezaji wote ambao wanaidai timu ya Yanga wanaenda kumaliziwa madeni yao yote wanayoidai Klabu ya Yanga.
Moja kati ya wachezaji amabao walikuwa kwenye mlolongo huo ni Golikipa Beno Kakolanya ambaye alisajiliwa kutoka Tanzania Prisons kuna taarifa kuwa ameahidiwa na Uongozi kuwa yeye na wachezaji wengine wanaoidai Yanga wanakwenda Kulipwa mwisho wa Mwezi Huu wa Kwanza.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: