Klabu Bingwa Nchini Tanzania , Klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu wake Mkuu Boniface Mkwasa “Master” imesema kuwa baada ya Mchezo wa Ruvu Shooting Jana wanajipanga kuhakikisha timu inakaa mapema Kambini kujiwinda na Mchezo dhidi ya Azam Fc siku ya Jumamosi.


Katika mchezo kati ya Ruvu Shooting na Yanga ulimaliza kwa ushindi wa bao 1 kwa 0 bao likifungwa na Kiungo wa pembeni Pius Charles Buswita.


Yanga itashuka dimbani kukipiga na Azam Fc January 27 wakati huo Azam jana ikipata Ushindi dhidi ya Prisons bao 2 kwa 0 na Kuongoza Ligi ikiwa Juu ya Simba wakati Yanga ikiwa nafasi ya Tatu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: