Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Mwigulu Nchemba ameagiza akamatwe na kupimwa akili ya mtu anayejiita nabii Tito aliyepo Dodoma na kuchunguzwa kama yupo sawasawa na kama yupo sawasawa afikishwe katika vyombo vya sheria ichukue mkondo wake.
Ameyasema hayo leo jiji Dar es salaam akiwa katika kanisa la wasabato mburahati wakati wa arambee ya ujenzi wa kanisa hilo.
Waziri Mwigulu amesema kila mtu ahaeshimu imani ya mwenzake bila kuingilia imani ya mwenzake na kutumia vizuri uhuru wa kuabudu bila kusababisha vurugu za kidini kwa kuchezea imani za watu.
"Nchi yetu hii tunaishi kwa kuheshimiana kwasababu tunaheshimu imani za watu ndio mana mpaka sasa bado tupo pamoja, wewe kama unajua wakristu wanaamini kama hakutakuwepo kanisa lipo kama baa au danguro wewe unaamua kutengeneza kanisa laina hiyo huko ni kutengeneza uchochezi ambayo inahatarisha hali ya amani kwa maana hiyo huo uhuru wa kuabudu watu wajue tafsiri vizuri" alisema waziri Mwigulu
Post A Comment: