WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe jana Januari 20, 2018 amemtembelea na kumjulia hali msanii wa filamu Wastara nyumbani kwake Tabata Sanene, Dar es Salaam.
Wastara kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mguu na yupo kwenye maandalizi ya safari kwenda India kwa matibabu zaidi.
Waziri Mwakyembe akiambatana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu na Katibu Mtendaji wa BASATA alimtakia kheri Wastara na kumkabidhi mchango wa Shs. 1,000,000/= (milioni moja).
Aidha, Mwakyembe aliwasihi wasanii na Watanzania kwa ujumla kumchangia Wastara kwa hali na mali ili aweze kupata fedha za kumwezesha kwenda India kwa matibabu zaidi
Post A Comment: